Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’ na ‘Ushairi Wenu’ Katika Gazeti la Taifa Leo.

  • Nyongesa Salyne; Sheila Wandera-Simwa; Wendo Nabea.
Keywords: Ushairi, mikondo, upya, ushairi wa magazetini

Abstract

Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi Agosti 31, 2019. Utafiti uliongozwa na nadharia ya kimtindo ya Leech na Short (2007) ili kuafikia lengo letu. Mihimili mitatu ya nadharia hii ilitumiwa ili kufanikisha lengo la mtafiti, nayo ni: Fasihi ni muundo wa lugha na kwa hivyo lazima matumizi ya lugha yazingatiwe, uhakiki wa kifasihi haupaswi kupuuza matumizi ya vipengele vya isimu lugha ikiwemo. Data iliyotumiwa katika utafiti ilikusanywa maktabani na mitandaoni kupitia usomaji wa tasnifu, vitabu, majarida na magazeti. Uteuzi sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua mashairi yaliyosheheni upya katika mikondo. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia kwa maelezo.Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba, mashairi ya ushairi wenu na sokomoko yanasheheni mikondo mipya ya utunzi ikiwemo: Matumizi ya Sheng’, usimulizi na kuwepo kwa mianzo ya kifomula. Mashairi yaliyotumika yalitolewa katika kumbi za Sokomoko na Ushairi Wenu ambazo ni kumbi zinazochapisha mashairi ya watunzi mbalimbali katika gazeti la Taifa Leo. Matokeo ya utafiti yalionesha namna mikondo mipya ya utunzi inaendelea kuibuliwa na watunzi wa mashair kila uchao. Mashairi yaliyotumika hapa hata hivyo, ni yale ya kiarudhi pekee kwani ndiyo yachapishwayo katika gazeti la Taifa Leo. Makala haya yatakuwa ya manufaa kwa walimu wa Kiswahili, wanafunzi na watafiti wengine wanaotafitia suala la upya katika utunzi wa mashairi.

Published
2020-12-15
Section
Articles