Itikadi na Uwezo wa Kijinsia katika Nyimbo za Taarab

  • Mary M. Malenya; Sheila Pamela Wandera Simwa; James O. Ogola Idara ya Fasihi, Lugha na Mawasiliano Chuo Kikuu cha Laikipia, Kenya
Keywords: Maneno muhimu: Itikadi, jinsia, uwezo, nyimbo

Abstract

Makala haya yalilenga kuchunguza itikadi inavyomsawiri mwanamke huku ikimpokonya uwezo wa kutekeleza majukumu sawa na mwanamume. Itikadi ndio huwaongoza watu namna wanavyotumia lugha na hivyo kudhihirisha mahusiano ya mamlaka. Usemi huu unadhibitisha hoja zinazowaongoza watunzi wa fasihi hivi kwamba lugha wanayotumia ndio hubainisha nafasi anayopewa mwanajamii. Suala hili liliwezeshwa kwa kuwepo na malengo mawili. Moja, kuchunguza utunzi na maudhui tawala katika nyimbo teule za taarab ili kubaini mafungamano ya masuala hayo na itikadi inayotawala. Pili, kuonyesha mahusiano ya uwezo kati ya mwanamke na mwanamume katika jamii kupitia nyimbo za taarab. Malengo haya yaliafikiwa kupitia uchanganuzi wa matumizi ya lugha katika nyimbo mbili teule za taarab ili kuonyesha usawiri wa mwanamke kwa kuzingatia itikadi na uwezo wa kijinsia. Nyimbo zilizochanganuliwa ni Daktari wa Mapenzi na VIP ambazo zimeimbwa na Mzee Yusuf akiwa na bendi ya Jahazi Modern Taarab nchini Tanzania.Vigezo vikuu vya uteuzi wa nyimbo hizi ni maudhui na lugha. Nadharia zilizotumika ni ufeministi wa Kiafrika inayorejelea masuala ya jinsia ya kike pamoja na Uchanganuzi Hakiki Usemi (UHU) itakayochunguza matumizi ya lugha. Data za makala haya zilikusanywa kwa kuchanganua nyimbo teule. Mtafiti alisikiza kanda ili kupata matini za kumfaa katika ukusanyaji data. Data iliyokusanywa ilifanyiwa unukuzi, kuainishwa, kupangwa, kuchanganuliwa na kufasiriwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia mbili zilizotumika katika utafiti huu. Data hiyo iliwasilishwa kwa njia ya maelezo.

Published
2020-05-30
Section
Articles