https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/issue/feed Editon Consortium Journal of Kiswahili 2022-12-29T21:26:20+00:00 Editon Consortium Publishing editor@editononline.com Open Journal Systems
Editon Consortium Journal of Kiswahili (ISSN: 2663-9289) (Online) is a Monthly, double-blind peer reviewed, open access, Journal published in East Africa, Kenya. The Journal publishes original scholarly research (empirical and theoretical), in form of case studies, reviews and analyses in Kiswahili Linguistic Studies.
https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/299 Sababu za kudondoshwa kwa fonimu za likwidi katika maneno teule 2022-12-29T21:26:20+00:00 Evans Kiplimo Cheruiyot cheruiyotevanskiplimo@gmail.com
Utafiti huu umelenga kuchunguza sababu za kudondoshwa kwa fonimu za likwidi katika maneno teule. Uchanganuzi huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi. Utafiti huu umetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kupitia kwa mbinu za kusoma na kudondoa. Ili kushughulikia tatizo la utafiti kikamilifu, utafiti huu ulitegemea aina tatu ya data. Kwanza, data ya maumbo yaliyopangwa upya kwa matumizi ya mbinu linganishi na uundaji ndani. Pili, data kutoka kwa Kamusi Kuu ya Kiswahili. Data hii iliteuliwa kimaksudi kwa sababu inaweza kutosheleza katika kushughulikia tatizo la utafiti. Data ya makala hii imechanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Makala hii ilibainisha kuwa ni vigumu kutenganisha vichocheo na sababu kamili za mabadiliko ya lugha. Pili, athari za mabadiliko ya lugha zinaweza kuingizwa kama maelezo ya sababu za mabadiliko ya lugha. Tatu, ilikuwa vigumu kubainisha mipaka baina ya sababu za kiisimu na kiisimu-jamii. Utafiti huu ulihitimisha kuwa kuwa mabadiliko mengine kama vile uchopekaji hutokea katika kiwango cha mofolojia ili kurekebisha makosa ya kimuundo katika lugha yanayosababishwa na badiliko la kwanza. Kando na haya, makala hii ilionyesha kuwa sheria ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi haina tija katika Kiswahili cha sasa. Utafiti huu unapendekeza kuwa Kuzuia uhomonimia na kuwepo kwa masalio ya kiisimu ni baadhi ya sababu zilizotolewa kueleza uzuiaji wa sheria.
2022-01-31T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/318 Athari za tafsiri ya jazanda na majazi kwa mawasiliano: Mfano wa tafsiri ya riwaya ya Shetani Msalabani 2022-12-29T21:26:13+00:00 Magugu V Njeru njeruwamagugu@gmail.com Robert W Oduori njeruwamagugu@gmail.com Mark M Kandagor njeruwamagugu@gmail.com
Makala hii imeangazia jinsi vipengele vya jazanda na majazi vimetumika katika riwaya ya Ng?g? wa Thiong’o ya Caitaani Mutharaba-ini iliyoandikwa awali katika lugha ya Kikuyu na baadaye kutafsiriwa kwa Kiswahili na Kiingereza na mwandishi mwenyewe. Caitaani Mutharaba-ini, Shetani Msalabani na Devil on The Cross ziliteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia umuhimu wake kama riwaya ya kwanza kuandikwa kwa Kikuyu na kutafsiriwa kwa Kiswahili na kiingereza, pamoja na ukwasi wake wa vipengele vya kijazanda na kimajazi. Sampuli ya data iliyochanganuliwa iliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwa mifano ya jazanda na majazi katika riwaya chanzi. Data iliyotumiwa katika kuandaa makala hii ilikusanywa kutokana na usomaji na uchanganuzi wa riwaya chanzi ya Kikuyu, tafsiri ya Kiswahili na ile ya Kiingereza. Data hii ilijikita kwa vipengele hivi vya jazanda na majazi. Uchanganuzi umejikita kwa jinsi mtafsiri alivyoshughulikia vipengele hivi kwa kuangazia jinsi vilivyotumika katika matini chanzi na namna vilivyohawilishwa katika tafsiri ya Kiswahili na ile ya Kiingereza. Katika kufanya hivi, utafiti umejiegemeza kwa nadharia ya baada ukoloni katika tafsiri hasa kipengele cha upekee wa lugha ya fasihi ya Kiafrika, iliyoandikwa na iliyotafsiriwa na kipengele cha uhusiano baina ya Lugha ya mtawaliwa na lugha ya mkoloni. Makala hii imebainisha kwamba licha ya kuwa nomino za pekee aghalabu hazitafsiriwi, katika miktadha ambamo zinabeba maana fiche kama ilivyo kwa majina ya kimajazi yaliyoangaziwa, huenda pana haja ya kutoa maelezo ili kufanikisha mawasiliano kamilifu.
2022-02-28T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/356 Kutathmini vipengele vya lugha vilivyotumiwa katika michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili 2022-12-29T21:26:04+00:00 Michael Kiguta mchlkiguta@yahoo.com
Utafiti huu unalenga kutathmini vipengele vya lugha vinavyotumiwa katika michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili. Nadharia iliyotumiwa ilikuwa ya umaumbo. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyo’uwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia kigezo cha matumizi ya lugha. Ulitafiti huu ulibaini kuwa lugha ya kisanii ilitumiwa katika tamthilia za shule za upili. Lugha iligawanywa kwa mifumo ya mbinu za kiishara na viambajengo vya umuundo. Mifumo ya ishara, maana ya lugha ya kiisimu na taashira za lugha zilitumiwa kujenga tamthilia. Tafiti hii inapendekeza tamthilia kujengwa vizuri kwa njia ya kisanaa kwa kutumia lugha yenye mvuto na mnato kusababisha ujumbe uliofaa, vile vile, wasanii wanahitaji kufanya utafiti mkubwa zaidi kuhusu sanaa ya lugha kwa kuwa ndiyo sehemu ya umuundo na unahitaji ufundi mkubwa.
2022-03-31T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/357 Kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii 2022-12-29T21:25:53+00:00 Wilfrida Kemuma winniekemuma@gmail.com
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data ulitumika katika kusanya data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumika kwa lengo la kupata sentensi ambazo hudhihirisha mageuzi. Data iliwasilishwa kwa njia za maelezo. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa muundo wa sentensi unahusu mpangilio wa viambajengo katika sentensi. Muundo wa virai ya sentensi sahili ya Ekegusii unategemea majopo ya maneno kisarufi. Majopo ya maneno yaliyotumika katika utafiti huu yanaweza kuainishwa katika makundi wawili: Jopo la leksia na jopo amilifu. Kuna categoria tano za maneno zilizoainishwa katika jopo leksia nazo ni nomino, kitenzi, kielezi, kivumishi na kihusishi. Jopo amilifu hutawaliwa na virai vibainishi, virai vipatanishi na virai shamirisho. Utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti zaidi zinaweza kufanywa kuhusu sentensi ambatano au changamano. Isitoshe, utafiti wa mageuzi unaweza kufanywa kwa lugha nyingine ili kueleza iwapo kuna matokeo tofauti.
2022-04-15T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/358 Matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya Said A. Mohamed 2022-12-29T21:25:44+00:00 Matthew Kwambai kwambai09@yahoo.com
Makala haya yanalenga kuangazia matumizi ya jazanda pamoja na uamilifu wake katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya Said A. Mohamed. Jazanda ni matumizi ya maneno ambayo yana fumbo huku yakitoa taswira ya aina Fulani. Said A. Mohamed ametumia jazanda kwa kazi zake kama Amezidi na Kitumbua Kimeingia Mchanga. Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga imetumia mbinu hii kwa njia ya kipekee. Nadharia iliyotumiwa katika kazi hii ni ya Umuundo ambao unasema kuwa kazi ya fasihi inakuwa na muundo ambao unahusisha fani ambazo zitaweza kutumika katika kuwasilisha ujumbe na hivyo maudhui huwa na uhusiano mkubwa sana na fani zitakazotumiwa kuyawasilisha. Utafiti ulifanywa maktabani kwa kuchambua Kitumbua Kimeingia Mchanga, vitabu tofauti na makala mitandaoni. Nakala hii ilipata matokeo kuwa kichwa cha kitabu hiki ni jazanda, pia, kulikuwa na jazanda ya bahari na yale yaliyokuwa yakifanyika kwenye bahari. Jazanda zote zilizotumika ziliweza kuendeleza maudhui kama vile: Mapenzi miongoni mwa vijana, Ndoa, Elimu, Mahusiano katika familia na jamii, Utamaduni na Dini. Uamilifu wa jazanda ni kudhihirisha jinsi mabadiliko yameathiri vijana na hivyo kwenda kinyume na utamaduni na wazee.
2022-04-20T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/359 Mikakati ya kimawasiliano katika matangazo ya ngono salama 2022-12-29T21:25:16+00:00 Douglas Nkumbo douglasnkumbo@yahoo.com
Makala haya yanalenga kuangazia mikakati ya kimawasiliano katika matangazo ya ngono salama. Masuala ya utangazaji wa mipira ya ngono ni baadhi ya mada ambazo ni mwiko katika tamaduni nyingi. Hii ni changamoto inayowakumba wanaoandaa matangazo ya ngono salama ili kukabiliana na changamoto hii ya kitamaduni. Usomi huu ulitathmini matangazo ya Durex katika mtandao wa Facebook fan page Kenya. Madhumuni yalikuwa: kuhakiki mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa katika matangazo ya Durex. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi (UHU) kwa kuzingatia miundo ya Fairclough 3D na muundo wa uchunganuzi wa picha wa Jankss. Muundo wa utafiti huu ni wa kiuthamano na kimaelezo. Sampuli ya data ilifanywa kimaksudi katika ukurasa wa Durex ambapo matangazo kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2018 yalichaguliwa. Kwa jumla matini 150 zilipakuliwa na kuhifadhiwa kieletroniki ili kuchanganuliwa. Matini hizi zilizua seti mbili za data; matini za picha na matini za maandishi. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa kuwasilisha maudhui ya umuhimu wa matumizi ya mipira ya ngono ni ya mawasiliano ya picha na mbinu za lugha katika viwango vya: fonolojia, leksia, sintaksia na semantiki ili kushawishi wateja. Utafiti huu utaongeza maarifa ya kiakademia katika Uchanganuzi Hakiki Usemi wa mada ambazo ni mwiko na mawasiliano ya afya. Utafiti huu utasaidia kuziba pengo la changamoto za kimawasiliano kwa wanaoandaa matangazo ya ngono salama ili kukabiliana na changamoto za kitamaduni kuhusu masuala ya ngono. Mwisho ni kuandaa sera za kuhamasisha umma kuhusu elimu ya ngono salama kupitia mitandao ya kijamii.
2022-04-25T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/360 Kuchanganua aina za mageuzi katika maneno ya sentensi sahili ya Ekegusii 2022-12-29T21:25:37+00:00 Wilfrida Kemuma winniekemuma@gmail.com
Utafiti huu unachanganua aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo. Data ilikusanywa maktabani kutumia kifaa cha kudondoa data, kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii. Ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi, mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa. Mbinu za maelezo zilitumika katika uwasilishaji wa data. Mchakato hufanywa kwa kufuata kanuni mahsusi zinazoitwa kanuni geuzi. Ugeuzi unafuata utaratibu maalum, haufanywi kiholela. Katika ugeuzi wa maumbo kuna sharti la ukaribu ambapo hakuna kiambajengo kinaweza kuhamishwa zaidi ya fundo funge mbili kutokana na matokeo ya utafiti huu. Kanuni zingine za uhamisho ni kanuni ya ufungami ambapo muundo wa kijenzi kilichofundwa unahitaji uamuliwe na neno tawala linalofaa. Kuna vilele kanuni ya ulafi, kanuni teta na kanuni hamishe. Mwisho kuna kanuni muundo virai, kanuni geuzi na kanuni za mofofonemiki. Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu aina zingine za mageuzi kama vile, geuzi hamishi swalifu, geuzi hamishi la yambwa tendewa katika lugha hii na hata lugha nyinginezo ili kukuza uwanja wa kisintaksia. Kuna uhamisho unaotokea kwa lugha zingine na siyo katika Ekegusii. Hizi pia zinaweza kufanyiwa utafiti. Tafiti zaidi zinaweza kufanyiwa mada hii kwa kutumia nadharia zingine ili kueleza ikiwa kutakuwa na matokeo tofauti.
2022-04-20T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/361 Maudhui yaliyotumiwa katika utunzi wa michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili 2022-12-29T21:25:30+00:00 Michael Kiguta mchlkiguta@yahoo.com
Utafiti huu ulilenga kutambua maudhui yaliyotumiwa katika utunzi wa michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyokuwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia vigezo mbalimbali vya matumizi ya maudhui. Makala hii ilibaini kuwa watunzi walitumia maudhui mbalimbali kukuza mada ya ukimwi. Baadhi ya maudhui ambayo yalitumiwa yalikuwa ya: mila na utamaduni, uhafidhina, asasi za ndoa, utabaka, utamauushi, uana, malezi, ufuska, uzinzi na kadhalika. Maudhui ulitumiwa kubeba ujumbe kuhusu ukimwi. Utafiti huu ulipendekeza kuwa maudhui yaliyojadiliwa yangefaa kuwa katika tajriba ya vijana ya  kila siku, maudhui ya ukimwi yangelijadiliwa bila kutumia mbinu ya kitanzia, ingekuwa bora kama tamthilia zingelijadili jinsi ya kuishi na waathiriwa wa ukimwi badala ya kuwatenga kama ilivyokuwa katika tamthilia ya Majuto, tamthilia ingetumika kwa njia ya ushawishi kuhusu ugonjwa wa ukimwi badala ya kulaumu na kukemea, mtunzi angeonyesha kuwa maafa si suluhu la matatizo bali ni kutorokea hali ngumu kwa njia ya kifantasia, ingekuwa bora kwa mtunzi kumuondoa katika tamthilia nzima kwa kuwa alifanaya kazi ya mtunzi iwe na udhaifu kisha kulihitajika watunzi wengi wa shule za upili wajitokeze ili tamthilia itumike vilivyo kama chombo mahsusi cha upashanaji wa ujumbe dhidi ya ukimwi.
2022-04-20T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/362 AMEZIDI IMEZIDI 2022-12-29T21:25:08+00:00 Matthew Kwambai kwambai09@yahoo.com
Makala haya yamelenga kuangazia muundo wa kipekee wa tamthilia hii na kuona jinsi muundo huu unavyowezesha uwasilishaji wa ujumbe wake. Tamthilia ya Amezidi ina muundo ambao ni tofauti na tamthilia nyingi za Kiswahili zilizoandikwa wakati mmoja. Nadharia iliyotumiwa katika kazi hii ni ya umuundo ambao unasema kuwa kazi ya fasihi inakuwa na muundo Fulani ambao unahusisha fani ambazo zitaweza kutumika katika kuwasilisha ujumbe na hivyo maudhui huwa na uhusiano mkubwa sana na fani zitakazotumiwa kuyawasilisha. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba, ambapo vitabu mbalimbali vilirejelewa huku yaliyomo katika tamthilia ya Amezidi yakihakikiwa. Matokeo yalidhihirisha kuwa Wahusika wawili na wa pekee ambao wanatekeleza majukumu yote katika tamthilia yote, mbinu kama vile uradidi na chuku zinatumiwa na wahusika hawa kuendeleza maudhui kama vile: umaskini, utegemeaji wa misaada na ndoto zisizoweza kutimizwa. Kutokana na haya yote inadhihirika kuwa tamthilia hii ya kukithiri mipaka ya uhalisia inakengeusha wahusika sawa na wasomaji wa tamthilia hii.
2022-04-25T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/363 Kutathmini mitindo mbalimbali ya kisanaa ilitumiwa katika michezo ya mashindano ya shule za upili yanayohusu ugonjwa wa ukimwi 2022-12-29T21:25:00+00:00 Michael Kiguta mchlkiguta@yahoo.com
Utafiti huu ulilenga kutathmini mitindo mbalimbali ya kisanaa ilitumiwa katika michezo ya mashindano ya shule za upili yanayohusu ugonjwa wa ukimwi. Nadharia ya semiotiki ilitumika katika utafiti huu. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyokuwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia vigezo mbalimbali vya matumizi ya lugha, maudhui na mbinu Michezo ya shule za upili ni mifupi mno (dakika 35 pekee), kwa hivyo kulihitajika mbinu za kimtindo na kimuundo ambazo zingeweza kusaidia kuwajenga wahusika na msuko wa hadithi uweze kuaminika. Tamthilia ya Majuto ilitumia maonyesho mengi mafupi mafupi ambayo hayakusaidia kuwajenga wahusika kikamilifu. Ingelifaa kama mtunzi angetumia onyesho moja na kuturudisha nyuma ya matukio kupitia mbinu rejeshi.
2022-04-25T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022 https://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/364 Kupambanua kanuni zinazotawala mageuzi katika sentensi sahili ya Ekegusii language in Kenya 2022-12-29T21:25:23+00:00 Wilfrida Kemuma winniekemuma@gmail.com
Utafiti huu unalenga kupambanua kanuni zinazotawala mageuzi katika sentensi sahili ya Ekegusii language in Kenya. Nadharia ya Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo uliongoza utafiti huu. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, kwa kutumia kifaa cha kudondoa data, vitabu teule vya Ekegusii ulitumika katika kusanya data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumika kwa lengo la kupata sentensi ambazo hudhihirisha mageuzi. Data iliwasilishwa kwa njia za maelezo. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa Ekegusii na sheria na kanuni zinazotawala mageuzi hayo. Mageuzi ya kisintaksia huleta mabadiliko mengi katika sentensi asili. Kanuni geuzi husababisha athari mahsusi katika sentensi kimuundo, kimofolojia na kifonetiki lakini kisemantiki sentensi huwa ni ile ile. Nadharia za Sintaksia Finyizi pamoja na nadharia Sarufi Geuza Maumbo ziliweza kuchanganua sentensi za Ekegusii kwa ukamilifu. Mapendekezo ya utafiti huu ni kufanya aina zingine za mageuzi kama vile, geuzi hamishi swalifu, geuzi hamishi la yambwa tendewa katika lugha hii na hata lugha nyinginezo ili kukuza uwanja wa kisintaksia. Kuna uhamisho unaotokea kwa lugha zingine nasiyo katika Ekegusii. Hizi pia zinaweza kufanyiwa utafiti. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni zile za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo. Tafiti zaidi zinaweza kufanyiwa mada hii kwa kutumia nadharia zingine ili kueleza ikiwa kutakuwa na matokeo tofauti.
2022-04-20T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2022