Vipengele Vya Ontolojia Katika Tamthiliya Za Kiswahili: Mashetani (1971) Na Kivuli Kinaishi (1990).

  • Rosalina Karata; Dr. Muusya Justus; Dr. Rose Mavisi. (1.2.3) Catholic University of Eastern Africa.
Keywords: Ontolojia, tamthiliya, kitaamuli, Mashetani, Kivuli Kinaishi.

Abstract

Makala haya yalilenga kuchambua vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya za Kiswahili: mfano wa Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990). Mbinu iliyotumika katika kukusanya data hii ni mbinu ya kitaamuli. Sampuli iliyotumika katika makala haya ni vitabu viwili vya tamthiliya ambavyo ni Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990). Tamthiliya hizi zitawakilisha zingine nyingi ambazo zimeandikwa na Ibrahimu Hussein na Said Mohamed. Mtafiti atajikita katika tamthiliya hizo mbili ili kuchambua vipengele vya ontolojia. Utafiti huu ulifanywa maktabani ambapo data ziliweza kukusanywa kwa kutumia mbinu ya udurusu maktaba. Mtafiti alipitia maandishi mbalimbali kutoka katika vitabu vilivyopo katika maktaba pamoja na wavuti ili kupata maelezo yaliyotosha kukidhi haja ya makala haya. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ambapo mtafiti aliitumia katika kuchambua vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya teule. Makala haya yatasaidia kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa kwa wale wasiofahamu kuchambua masuala ya kiontolojia katika fasihi andishi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa kutoka katika tamthiliya ya Mashetani na Kivuli Kinaishi vimeweza kusawiri ontolojia ya Kiafrika na nafasi yake kwa jamii.

Published
2021-09-30
Section
Articles