Mitazamo ya Walimu wa Fasihi ya Kiswahili Kuhusu Ufaafu wa Hadithi Fupi Teule kwa Bibliotherapia.

  • Rose Mavisi; Dr. Gwachi Mayaka; Prof. Wendo Nabea
Keywords: Bibliotherapia, mitazamo, walimu, hadithi fupi.

Abstract

Makala haya yalilenga kutathmini mitazamo ya walimu wa fasihi kuhusu ufaafu wa hadithi fupi kutumika kama bibliotherapia ya matatizo yanayowakumba wanafunzi. Utafiti huu ulipata matini yake kutoka kwa hadithi fupi teule zifuatazo; Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine (2004), Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine (2007), Kiti cha Moyoni na hadithi nyingine (2007) na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016). Mwalimu alifaa kuteua hadithi mwafaka kwa mwanafunzi kwa kuzingatia umri, maudhui yanayojitokeza na usawiri wa wahusika waliopitia matatizo yaliyo sawa na yale ya wanafunzi husika. Mbinu iliyotumiwa kukusanya data hii ni hojaji wazi na funge. Mtafiti aliwahoji walimu wa fasihi ya Kiswahili katika shule za upili Kaunti ya Nairobi. Mtafiti alitumia seti mbili za hojaji kama vifaa vya kukusanya data ya walimu. Hojaji zilizotolewa kwa walimu ishirini na wanane zilikuwa na maswali funge na huru. Maswali funge yalikuwa na muundo maalum ili kumpa mtafiti nafasi ya kupata majibu yasiyo na maelezo ya ndani. Maswali huru yalimpa mtafiti uwezo wa kupata data yenye undani kuhusu mitazamo ya walimu wa fasihi ya Kiswahili kuhusu matumizi ya hadithi fupi teule za Kiswahili kama bibliotherapia kwa wanafunzi. Nadharia ya NMMM yake Rosenblatt (1995) ilitumika katika kuchanganuakazi hii.

Published
2021-06-05
Section
Articles