Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.695

Authors

Keywords:

Maendeleo, mabadiliko ya tabianchi, Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME), tamthilia, uongozi

Abstract

Swahili

Lengo la makala hii ni kuchunguza udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016). Mpango wa MME umekumbatiwa na wasomi, wataalamu, mashirika na serikali mbalimbali duniani kwa kuwa ni njia ya kuafikia maendeleo. Waandishi wa fasihi wameshughulikia masuala ya maendeleo katika kazi zao. Fasihi kupitia utanzu wa tamthilia ina nafasi muhimu ya kuchangia uafikiaji wa MME kwa kuyaangazia. Utafiti huu ni wa kithamani na uliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt (1980) na kuendelezwa na Brizee na Tompkins (2012). Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Data ilikusanywa kupitia mbinu ya unukuzi. Data kuhusu namna MME yanavyodhihirika katika tamthilia teule iliibuliwa kupitia wahusika, uumbaji wa mandhari na maudhui. Data hii ilipangwa kisha kuchanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia ya Shamba la Halaiki iliyoandikwa na Daniel Okello, 2016 iliteuliwa. Tamthilia hii iliteuliwa kwa msingi kuwa inaangazia MME na imeandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2026 ambao ni kipindi cha utekelezaji wa mpango wa MME. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya maandishi. Matokeo yanaonyesha kuwa tamthilia teule inadhihirisha MME kupitia vipengele vya kifasihi kama wahusika, mandhari na maudhui, hivyo kujitokeza kama jukwaa muhimu la kujadili maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Hata hivyo, imebainika kuwa baadhi ya malengo hayajaangaziwa ipasavyo, hususan L2, L8, L9, L10, L12 na L14. Makala inapendekeza waandishi wa fasihi kuzingatia zaidi malengo haya ili kuimarisha mchango wa fasihi katika kuendeleza ajenda ya maendeleo endelevu.

English

The aim of this article is to examine the manifestation of Sustainable Development Goals (SDGs) in the play Shamba la Halaiki (Okello, 2016). The SDG agenda has been embraced by scholars, professionals, organisations, and governments worldwide as a pathway to achieving development. Literary authors have addressed development issues in their works. Literature—through the genre of drama—plays an important role in contributing to the attainment of SDGs by highlighting them. This study is qualitative in nature and was guided by the New Historicism theory, initiated by Stephen Greenblatt (1980) and later developed by Brizee and Tompkins (2012). An analytical research design was employed. Data were collected through textual analysis. Data on how SDGs are manifested in the selected play was derived from characters, setting, and themes. The data were organised and analysed using content analysis. Through purposive sampling, the play Shamba la Halaiki, written by Daniel Okello (2016), was selected. The play was chosen on the basis that it addresses SDGs and was written within the period 2016–2026, which aligns with the implementation phase of the SDG agenda. Findings are presented in descriptive form. The results indicate that the selected play reflects SDGs through literary elements such as characters, setting, and themes, thus emerging as an important platform for discussing social, economic, and environmental development. However, it has been observed that some goals are not adequately addressed, particularly SDGs 2, 8, 9, 10, 12, and 14. The article recommends that literary authors give more attention to these goals in order to strengthen the contribution of literature to the advancement of the sustainable development agenda.

 

Keywords: Development, climate change, sustainable development goals (SDGs), drama, leadership.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-01-13

How to Cite

Ogonda, S. S. (2026). Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 13–25. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.695

Issue

Section

Articles