Mikakati ya Kimawasiliano katika Matangazo ya Ngono Salama.

  • Douglas Nkumbo Laikipia University, Kenya.
Keywords: Matangazo, ngono salama, mawasiliano ya picha, mbinu za lugha.

Abstract

Makala haya yanalenga kuangazia mikakati ya kimawasiliano katika matangazo ya ngono salama. Masuala ya utangazaji wa mipira ya ngono ni baadhi ya mada ambazo ni mwiko katika tamaduni nyingi. Hii ni changamoto inayowakumba wanaoandaa matangazo ya ngono salama ili kukabiliana na changamoto hii ya kitamaduni. Usomi huu ulitathmini matangazo ya Durex katika mtandao wa Facebook fan page Kenya. Madhumuni yalikuwa: kuhakiki mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa katika matangazo ya Durex. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi (UHU) kwa kuzingatia miundo ya Fairclough 3D na muundo wa uchunganuzi wa picha wa Jankss. Muundo wa utafiti huu ni wa kiuthamano na kimaelezo. Sampuli ya data ilifanywa kimaksudi katika ukurasa wa Durex ambapo matangazo kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2018 yalichaguliwa. Kwa jumla matini 150 zilipakuliwa na kuhifadhiwa kieletroniki ili kuchanganuliwa. Matini hizi zilizua seti mbili za data; matini za picha na matini za maandishi. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa kuwasilisha maudhui ya umuhimu wa matumizi ya mipira ya ngono ni ya mawasiliano ya picha na mbinu za lugha katika viwango vya: fonolojia, leksia, sintaksia na semantiki ili kushawishi wateja. Utafiti huu utaongeza maarifa ya kiakademia katika Uchanganuzi Hakiki Usemi wa mada ambazo ni mwiko na mawasiliano ya afya. Utafiti huu utasaidia kuziba pengo la changamoto za kimawasiliano kwa wanaoandaa matangazo ya ngono salama ili kukabiliana na changamoto za kitamaduni kuhusu masuala ya ngono. Mwisho ni kuandaa sera za kuhamasisha umma kuhusu elimu ya ngono salama kupitia mitandao ya kijamii.

Published
2022-04-25
Section
Articles