Uchambuzi wa Changamoto Zinazotokana na Kutohifadhi Mazingira: Tathmini ya Uwasilishaji wA Vipindi vya Shamba Shape-Up na Citizen Planet Katika Runinga ya Citizen
DOI:
https://doi.org/10.51317/h9wd2c89Keywords:
Bioanuwai, ikolojia, tabianchi, uhifadhi wa mazingiraAbstract
Swahili
Utafiti huu unalenga kubainisha changamoto zinazotokana na kutohifadhi mazingira zinazowasilishwa katika vipindi vya Shamba Shape-Up na Citizen Planet, kuchambua namna vipindi hivyo vinavyowasilisha changamoto hizo, na kuchunguza athari zake kama zinavyojitokeza katika maudhui ya vipindi hivyo. Uhifadhi wa mazingira ni suala muhimu katika kukuza maendeleo endelevu na ustawi wa jamii; hivyo, mawasiliano ya mazingira kupitia vyombo vya habari yana umuhimu mkubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii. Kutohifadhi mazingira kumeendelea kusababisha changamoto mbalimbali zinazohatarisha maendeleo endelevu na ustawi wa jamii. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki-Ikolojia na ulitumia mkabala wa kimaelezo uliotegemea uchambuzi wa maudhui. Data zilipatikana kupitia uchambuzi wa vipindi teule vilivyochaguliwa kwa kutumia usampulishaji wa makusudi. Matokeo yalionyesha kuwa vipindi hivyo vinaibua changamoto mbalimbali, zikiwemo ukataji miti ovyo, uchafuzi wa mazingira, mmomonyoko wa udongo, upungufu wa rasilimali za maji, kupungua kwa rutuba ya ardhi, kuharibika kwa bioanuwai, na athari za mabadiliko ya tabianchi. Changamoto hizo zinawasilishwa kwa kutumia mifano ya maisha halisi, ushuhuda wa wahusika, na maelezo ya kitaalamu yanayobainisha uhusiano kati ya shughuli za binadamu na uharibifu wa mazingira. Aidha, athari zinazojitokeza ni pamoja na kupungua kwa uzalishaji wa kilimo, uhaba wa maji, kuharibika kwa mifumo ya ikolojia, kuhatarishwa kwa bioanuwai, na kuzorota kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Makala hii inahitimisha kuwa vipindi hivi vina mchango katika kuibua uelewa kuhusu changamoto na athari za kutohifadhi mazingira, na vinaweza kutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira.
English
This study aimed to identify the environmental challenges resulting from environmental degradation as presented in the television programmes Shamba Shape-Up and Citizen Planet, analyse how these programmes communicate such challenges, and examine the impacts of environmental degradation as reflected in their content. Environmental degradation continues to cause numerous challenges that threaten sustainable development and the well-being of society. The media play a vital role in raising public awareness of these challenges by providing environmental information and education. The study was guided by the Ecocriticism Theory and employed a descriptive research approach based on content analysis. Data was collected through the analysis of purposively selected episodes of Shamba Shape-Up and Citizen Planet and analysed using the content analysis technique. The findings revealed that the programmes highlight a range of environmental challenges arising from environmental degradation, including deforestation, environmental pollution, soil erosion, water resource depletion, declining soil fertility, biodiversity loss, and the impacts of climate change. Furthermore, the analysis demonstrated that these challenges are communicated through real-life examples, participants' testimonies, and expert explanations that illustrate the relationship between human activities and environmental degradation. The findings also indicated that the consequences of environmental degradation include reduced agricultural productivity, water scarcity, ecosystem degradation, threats to biodiversity, and the deterioration of social and economic development. The study concludes that Shamba Shape-Up and Citizen Planet make a significant contribution to raising public awareness of the challenges and consequences of environmental degradation. Consequently, these programmes can serve as effective tools for educating the public and promoting the sustainable use and conservation of environmental resources.
Downloads
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Joyce Njau Wambui, Rose Mavisi, Douglas Nkumbo

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.