Uchanganuzi wa Maudhui Kihalisia katika Nyimbo Teule za Ohangla za Prince Indah Nchini Kenya

Authors

  • Millicent Apondi Oloo Catholic University of Eastern Africa, Kenya , Catholic University of Eastern Africa, Kenya https://orcid.org/0009-0001-6167-6093
  • Harrison Onyango Ogutu
  • Mary Malenya

DOI:

https://doi.org/10.51317/nn48wq83

Keywords:

Jamii, maudhui, nyimbo za Ohangla, uhalisia, Waluo

Abstract

Makala hii inalenga kubainisha maudhui yanayojitokeza katika nyimbo teule za Ohangla za Prince Indah na namna yanavyoakisi uhalisia wa maisha ya jamii ya Waluo. Ingawa Ohangla ni mojawapo ya aina maarufu za muziki wa asili nchini Kenya, maudhui ya nyimbo zake za kisasa, hususan za msanii mmoja, hayajapata uchunguzi wa kina wa kitaaluma. Makala hii inalenga kubainisha maudhui yanayojitokeza katika nyimbo teule za Ohangla za Prince Indah na namna yanavyoakisi uhalisia wa maisha ya jamii ya Waluo. Kwa kutumia Nadharia ya Uhalisia, hasa Mhimili wa Uhalisia wa Maisha ya Kila Siku, nyimbo 12 ziliteuliwa kimakusudi kutoka nyimbo 30 alizoimba kati ya 2020 na 2025, kwa kuzingatia utajiri wa maudhui, mbinu za lugha za kisanaa na dhima ya kijamii. Nyimbo hizo zilisikilizwa zaidi ya mara moja, zikatafsiriwa kutoka Kijaluo kwenda Kiswahili, na data zikachanganuliwa kimaudhui kwa kufuata hatua za Braun na Clarke (2006). Matokeo yalibainisha maudhui matano makuu yanayoingiliana: mapenzi na uhusiano wa kimahaba; imani na utegemezi kwa Mungu; wivu, dharau na uvumilivu wa kijamii; ndoa, mahari na heshima ya familia; pamoja na falsafa ya maisha ya mara moja. Matokeo yanaonesha kuwa nyimbo hizi huakisi uzoefu wa maisha ya jamii ya Waluo huku zikiunganisha vipengele vya kimila na vya kisasa. Utafiti unapendekeza uchunguzi wa nyimbo za wasanii wengine wa Ohangla na wa maudhui ya kiimani kwa mitazamo ya kiteolojia au kiishara. Kwa ujumla, makala inaonesha mchango wa muziki wa asili katika kuwasilisha uzoefu wa kijamii na kiutamaduni katika enzi ya majukwaa ya kidijitali.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2026-09-23

Issue

Section

Articles

How to Cite

Uchanganuzi wa Maudhui Kihalisia katika Nyimbo Teule za Ohangla za Prince Indah Nchini Kenya. (2026). Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 147-155. https://doi.org/10.51317/nn48wq83

Most read articles by the same author(s)