Uhawilishaji wa Utamaduni na Mwachano wake katika Tafsiri ya Fasihi: Tathmini ya Athari katika Maisha ya Siri na Hadithi Nyingine
Keywords:
Mwachano wa kitamaduni, tafsiri ya fasihi, uhawilishaji wa utamaduni, ulinganifu wa kidhima, utotafsirikajiAbstract
Makala hii inachunguza uhawilishaji wa utamaduni katika tafsiri ya fasihi na jinsi unavyoathiri maana na ujumbe wa matini kwa hadhira lengwa. Utafiti unalinganisha matini chanzi Secret Lives and Other Stories na tafsiri yake ya Kiswahili Maisha ya Siri na Hadithi Nyingine. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo na uchanganuzi wa matini, ambapo dondoo tano zilizochaguliwa kimakusudi kutoka hadithi mbili, Mubenzi Tribesman (Mubenzi) na A Mercedes Funeral (Mazishi ya Benzi), zilichambuliwa ili kubainisha uhawilishaji wa vipengele vya kitamaduni kama nahau, taswira, marejeleo ya kijamii na istilahi za kiimani. Matokeo yanaonyesha kuwa baadhi ya dhana na taswira za kitamaduni zilipitia mabadiliko ya maana au kupoteza athari yake kutokana na ukosefu wa visawe vya moja kwa moja. Aidha, matumizi ya mikakati ya uenyejishaji na ugenishaji yalichangia ama kupunguza uzito wa kitamaduni wa matini chanzi au kurahisisha uelewekaji kwa wasomaji wa Kiswahili. Pia, marejeleo ya kihisia na mamlaka ya kijamii yalirekebishwa ili kuendana na utamaduni lengwa, jambo lililosababisha mwachano wa kidhima na kubadilika kwa athari ya ujumbe. Makala inahitimisha kuwa tafsiri ya fasihi ni mchakato wa uundaji upya wa utamaduni, ambapo maamuzi ya mtafsiri yanaweza kuhifadhi au kubadilisha mguso wa kitamaduni wa matini chanzi. Utafiti unapendekeza watafsiri kudumisha uwiano kati ya uelewekaji wa ujumbe na uhifadhi wa vipengele muhimu vya utamaduni ili kupunguza mwachano wa maana.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2026 Masibo Simon, Mosol Kandagor, Samuel Obuchi

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.

