Matumizi ya Mtindo na Mbinu za Lugha katika Nyimbo za Kampeni za Urais Nchini Kenya (2002–2022)

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.726

Authors

Keywords:

Diskosi, kampeni, lugha, nyimbo, siasa

Abstract

Swahili

Makala hii inachunguza matumizi ya mtindo na mbinu za lugha katika nyimbo za kampeni za urais nchini Kenya kati ya mwaka 2002 na 2022. Tofauti na tafiti nyingi zilizojikita katika hotuba na mikutano ya kisiasa, utafiti huu unazingatia nyimbo za kampeni kama maandiko ya kisiasa yenye ushawishi mkubwa katika kujenga mitazamo ya wapiga kura. Nyimbo nane (8) zilichaguliwa kimaksudi kutoka chaguzi tano za urais kwa kuzingatia umaarufu, usambazaji mpana kupitia vyombo vya habari, na mchango wake katika kujenga taswira ya wagombea. Data ilikusanywa kati ya Januari na Juni 2024 na kuchambuliwa kwa kutumia uchambuzi wa maudhui kupitia mbinu ya kithamano ya kimaelezo. Matokeo yanaonyesha kuwa mbinu za lugha kama takriri, mwito-na-mwitiko, sitiari, methali, nahau, chuku, lugha ya hisia na uchanganyaji wa ndimi zilitumiwa kimkakati kuhamasisha wapiga kura na kuimarisha ujumbe wa kisiasa. Takriri na mwito-na-mwitiko zilikuza mshikamano na ushiriki wa hadhira, huku sitiari, methali na nahau zikijenga matumaini, kuhalalisha ujumbe na kuimarisha uhusiano wa kijamii. Aidha, uchanganyaji wa Kiswahili na lugha za kimaeneo uliimarisha utambulisho wa pamoja, na nyimbo zenye jazanda na lugha ya hisia zilihusishwa na ongezeko la hamasa katika mikutano ya kampeni. Utafiti unahitimisha kuwa matumizi ya lugha katika nyimbo za kampeni ni ya kimkakati na yana mchango mkubwa katika kuunda mitazamo na kuelekeza maamuzi ya kisiasa. Unapendekeza tafiti zijazo zichunguze athari za nyimbo hizi kwa makundi mbalimbali ya kijamii na kuhimiza uwajibikaji katika matumizi ya lugha ya kampeni.

English

This paper examines the use of stylistic and linguistic techniques in presidential campaign songs in Kenya between 2002 and 2022. Unlike many studies that have focused on political speeches and rallies, this study considers campaign songs as political texts with substantial influence in shaping voters' attitudes. Eight (8) songs were purposively selected from five presidential elections on the basis of their popularity, wide dissemination through the media, and their contribution to constructing candidates' public image. Data were collected between January and June 2024 and analysed using content analysis through a qualitative descriptive approach. The findings reveal that linguistic techniques such as repetition, call-and-response, metaphor, proverbs, idioms, hyperbole, emotive language, and code-mixing were strategically employed to mobilise voters and reinforce political messages. Repetition and call-and-response fostered solidarity and audience participation, while metaphor, proverbs, and idioms cultivated hope, legitimised messages, and strengthened social bonds. Furthermore, the mixing of Kiswahili with local languages reinforced collective identity, and songs featuring imagery and emotive language were associated with heightened enthusiasm at campaign rallies. The study concludes that the use of language in campaign songs is strategic and makes a significant contribution to shaping public attitudes and directing political decisions. It recommends that future research investigate the effects of these songs on various social groups and promote accountability in the use of campaign language.

Keywords: Campaign, discourse, language, politics, songs

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-07-24

How to Cite

Carlpeters, M. A., Obuchi, S. M., & Kandagor, M. (2026). Matumizi ya Mtindo na Mbinu za Lugha katika Nyimbo za Kampeni za Urais Nchini Kenya (2002–2022). Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 62–74. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.726

Issue

Section

Articles