Yaliyomo katika Jukwaa la YouTube kama Wenzo wa Kufundishia Kiswahili katika Elimu ya vyuo vikuu: Ushahidi kutoka Chuo Kikuu cha Kibabii, Kenya
Keywords:
Elimu ya vyuo vikuuu, Kiswahili, maudhui ya kidijitali, wenzo wa ufundishaji, YouTubeAbstract
Swahili
Makala hii ililenga kuchunguza upatikanaji wa YouTube katika ufundishaji wa Kiswahili, kubainisha matumizi yake katika ufundishaji huo, na kuchunguza yaliyomo kwenye YouTube kama chombo cha kufundishia Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kibabii. Utafiti ulitokana na matumizi ya teknolojia za kidijitali zinazobadilisha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji katika vyuo vikuu, huku YouTube ikitokea kama moja ya majukwaa yanayotumika kwa upana kusambaza maudhui ya kielimu. Utafiti uliongozwa na mkabala mseto wa mbinu sambamba. Data za kiai zilikusanywa kutoka kwa wahadhiri 10 na wanafunzi 87 kwa kutumia hojaji. Aidha, video 44 za YouTube zilizotumika kama zana za kufundishia Kiswahili zilifanyiwa uchambuzi wa maudhui. Washiriki waliteuliwa kwa kutumia mbinu za usampulishaji za nasibu na za kimakusudi kulingana na sifa za makundi husika. Data za kiasi zilizopatikana zilichanganuliwa kwa takwimu za maelezo (masafa na asilimia), huku data za ubora na maudhui ya video zikifanyiwa uchambuzi wa dhamira na uchambuzi wa maudhui. Matokeo yalionyesha kuwa YouTube inapatikana na kutumika kwa kiwango kikubwa katika ufundishaji wa Kiswahili, na ina maudhui yanayohusiana na matamshi, sarufi, msamiati, fasihi na mawasiliano ambayo huongeza uelewa wa wanafunzi, ushiriki wao na ujifunzaji wa kujitegemea. Makala hii inahitimisha kuwa YouTube ni chombo muhimu cha kufundishia Kiswahili ikiwa maudhui yake yatahifadhiwa na kutumika kwa mujibu wa malengo ya ufundishaji. Utafiti unachangia maarifa kuhusu matumizi ya YouTube katika ufundishaji wa Kiswahili unaonyesha kuwa ubora wa maudhui, ulinganifu wake na mtaala, pamoja na uwezo wa walimu kuyachagua na kuyatumia kwa ufanisi, ndizo nguzo za matumizi yenye tija ya YouTube katika elimu ya vyuo vikuu.
English
This study sought to examine the accessibility of YouTube in the teaching of Kiswahili, identify its use in Kiswahili instruction, and analyse YouTube content as a teaching resource for Kiswahili at Kibabii University. Despite the increasing use of digital technologies, there remains a shortage of studies examining YouTube content and its contribution as a teaching resource for Kiswahili in higher education institutions in Kenya. The study was guided by a convergent parallel mixed-methods research design. Quantitative data were collected from 10 lecturers and 87 students using questionnaires. In addition, 44 YouTube videos used as Kiswahili teaching resources were analysed through content analysis. Participants were selected using both random and purposive sampling techniques based on the characteristics of the respective target groups. Quantitative data were analysed using descriptive statistics (frequencies and percentages), while qualitative data and video content were analysed using thematic analysis and content analysis. The findings revealed that YouTube is readily accessible and widely used in Kiswahili teaching. Its content covers pronunciation, grammar, vocabulary, literature, and communication, thereby enhancing learning, student engagement, and independent learning. The study concludes that YouTube is a valuable resource for teaching Kiswahili, provided that its content is carefully evaluated and used in accordance with instructional objectives. Ultimately, the study is fundamental, as it contributes to the existing body of knowledge on the use of YouTube in Kiswahili instruction by demonstrating the importance of content quality, curriculum alignment, and teachers’ ability to select and integrate appropriate videos effectively.
Keywords: Digital content, higher education, Kiswahili, teaching resources, YouTube
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2026 VITALIS SAKITI, Gladys Kinara, Amukowa Deborah

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.

