Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.713

Authors

Keywords:

Anafora, katafora, mshikamano, uhusiano, urejelezi

Abstract

Swahili

Makala hii inabainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Suala la urejelezi limechunguzwa na wasomi wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanywa kwa kina kuhusu aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu iliyoendelezwa na Halliday (1985, 1994, 1999), Halliday na Matthiessen (2004) na Matthiessen (2013) kwa kuangazia mtazamo wa Halliday na Hasan (1976). Aidha, Nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Wilson (2003) na Wilson na Sperber (2002) ilitumika kama nadharia changizi katika kufafanua jinsi wasomaji wanavyofikia maana tambuzi katika matini. Mbinu ya makala hii ni ya kimaelezo. Sampuli ya utafiti ilikuwa ya kimakusudi, ambapo nakala 30 za Habari za Kaunti zilizo na aina mbalimbali za urejelezi zilichaguliwa. Data iliyotumika katika makala hii ilikusanywa kutoka gazeti la Taifa Leo kati ya mwezi wa Juni na Julai 2020 kwa ajili ya tasnifu ya uzamili iliyoshughulikia suala la Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa ili kubainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zilivyotumika kuleta mshikamano katika matini. Matokeo yameonyesha kuwa aina mbalimbali za urejelezi zimetumika kuleta mshikamano katika matini. Makala hii inaonyesha kuwa urejelezi wa kiendofora, urejelezi nafsi, urejelezi wa kuashiria na urejelezi wa kulinganisha umetumika katika Habari za Kaunti ili kuleta mshikamano katika matini. Data ya makala hii imewasilishwa kwa kutumia maelezo ili kuonyesha jinsi aina mbalimbali za urejelezi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Utafiti huu utawafaa wasomaji wa gazeti katika kutambua na kufasiri aina mbalimbali za urejelezi kwa njia inayofaa ili kupata habari iliyokusudiwa na mwandishi.

English

This paper examines reference types used to bring cohesion in the Taifa Leo newspaper. Analysis of reference types used in news articles has become a research backdrop. However, only a few studies have been carried out on the reference types used to provide cohesion in the Taifa Leo newspaper. This work was based on Functional Grammar Theory, which was proposed and advanced by Halliday (1985, 1994, 1999), Halliday and Matthiessen (2004) and Matthiessen (2013) in reference to Halliday and Hasan (1976). Also, Relevance Theory, proposed and advanced by Wilson (2003) and Wilson and Sperber (2002), was used to demonstrate how readers arrive at cognitive meaning in a text. A descriptive qualitative research design was employed to examine the reference types used in Habari za Kaunti in Taifa Leo newspaper to foster cohesion. The data of this study were collected between June and July 2020 for a master's thesis titled ‘Urejelezi katika gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki. Data were collected using purposive sampling, in which 30 Habari za Kaunti articles with different reference types were selected for this study. While analysing the reference types, it was found that endophoric, personal, demonstrative and comparative references were used in Habari za Kaunti to bring cohesion in the text. The present study benefits news readers by helping them identify and interpret reference types correctly, ensuring they obtain the information intended by the writer.

Keywords: Anaphor, cataphor, cohesion, reference, relevance

 

 

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-06-22

How to Cite

Kirui, S. K. (2026). Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 26–34. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.713

Issue

Section

Articles