Athari za Nyimbo za Kilimo katika Jamii ya Wasukuma katika Jamii za Leo

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.662

Authors

Keywords:

Athari, nyimbo, jamii, kilimo, utamaduni.

Abstract

Swahili

Makala hii inahusu athari za nyimbo za kilimo katika jamii ya Wasukuma kwa kujikita katika wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, katika muktadha wa jamii ya leo. Kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, kumekuwa na hofu kuwa nyimbo za kilimo hazina umuhimu katika jamii ya sasa. Hivyo, makala hii inalenga kuweka bayana umuhimu wa nyimbo hizo katika jamii ya leo. Utafiti huu umetumia nadharia ya Usosholojia wa Fasihi iliyomwongoza mtafiti katika ukusanyaji na uchambuzi wa nyimbo za kilimo. Aidha, nadharia ya Utendaji wa Maigizo imemwezesha mtafiti kutambua namna nyimbo hizo zinavyotekelezwa miongoni mwa hadhira na kuainisha tabia zao. Usampulishaji wa makusudi ulitumika katika kuchagua vikundi vya kilimo vilivyosajiliwa katika kata, vyenye jumla ya watu themanini (80), na mbinu ya usampulishaji wa kubahatisha ilitumika kupata sampuli iliyosaidia kutoa taarifa zilizohitajika kuhusu athari za nyimbo za kilimo katika jamii ya Wasukuma. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, hojaji, ushiriki na ushuhudiaji. Vifaa kama kamera, kinasa sauti, redio na kanda vilitumika katika ukusanyaji wa data hizo. Kupitia mbinu hizo, mtafiti aliweza kukusanya data zilizohitajika na kukidhi malengo ya utafiti. Katika lengo la kwanza, nyimbo zilizobainishwa ni pamoja na nyimbo za kupanda, kupalilia na kuvuna. Lengo la pili lilihusu kubainisha dhima za nyimbo hizo, zikiwamo kuhamasisha jamii katika kazi, kukuza talanta na sanaa, kuburudisha jamii, kukuza ushirikiano miongoni mwa wanajamii, kuonyesha hisia za mtu binafsi, pamoja na kuendeleza na kueneza utamaduni wa jamii husika. Lengo la tatu lilihusu kutoa mapendekezo, ambapo ilipendekezwa kuwa nyimbo za jamii ya Wasukuma zihifadhiwe katika machapisho na mitandao mbalimbali ili ziweze kuonwa na vijana wa sasa na kuthaminiwa kama ilivyokuwa hapo awali miongoni mwa wanajamii.

English

The purpose of this article is to examine the effects of agricultural songs in the Sukuma community in contemporary society, specifically in Kwimba District, Mwanza City. Due to the development of science and technology, there is a growing concern about the decline in the use and relevance of Sukuma agricultural songs in modern society. This study highlights the continued importance of these songs in contemporary life. The study employed literary sociological theory to collect and analyse songs from the community, while performance theory in drama was used to identify performance behaviours among audiences. Purposive sampling was applied to identify registered agricultural groups in ward offices, and eighty respondents were selected through random sampling to represent members of these groups. Data were collected through interviews, participation, observation, and questionnaires, using instruments such as a camera, sound recorder, audio tape, and radio. The findings revealed three main categories of agricultural songs: planting, weeding, and harvesting songs. The study further established that these songs motivate people to work, provide entertainment, promote solidarity, express emotions, develop talents, and preserve cultural values. The study recommends preserving Sukuma agricultural songs in written form and on various social media platforms to ensure accessibility for younger generations and to promote their continued use and appreciation.

 

Keywords: Agriculture, contemporary, impact, importance, society, songs

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-02-27

How to Cite

Kanwa, O. (2026). Athari za Nyimbo za Kilimo katika Jamii ya Wasukuma katika Jamii za Leo. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 1–12. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.662

Issue

Section

Articles