Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Keywords:
Dhamira, sanaa, visasuli, wahayaAbstract
Swahili
Sanaa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku katika kabila la Wahaya. Umuhimu wa sanaa katika kabila la Wahaya unatokana na utajiri mkubwa walionao katika fasihi simulizi hususani visasuli. Licha ya utajiri huo bado inaonesha kuwa maandiko mengi ya kisanaa na kihistoria hayakuandikwa hali iliyosababisha kutokuwapo kwa tafiti za kutosha kuhusu visasuli vya kabila la Wahaya. Makala hii imechunguza dhamira zinazojengwa na vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya. Sababu ya uchunguzi huu ni kwamba vipengele vya sanaa vimekuwa vikichunguzwa kwa ujumla sana katika kazi za fasihi bila ubayana unaoonesha namna vipengele hivyo vinavyojenga dhamira katika visasuli, hususani visasuli vya Wahaya. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano. Mjadala wa kimsingi katika Makala hii umekitwa na kuongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji iliyoasisiwa na Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish (1980) James Tompkins (1980), Haus Robert Jauss (1982) na Robert Holub (1984), katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya vinatumika kujenga dhamira. Dhamira hizo ni pamoja na matumizi ya vifaa jadi wakati wa kula, kuonesha thamani ya kitu unachokimiliki, kuharibika kwa maadili, kuendeleza utamaduni, uzazi, mahari, na huruma kwa wahitaji.
English
Art constitutes a central aspect of daily life among the Haya people. Its significance derives from the community’s rich heritage in oral literature, particularly in myths. Despite this wealth, many artistic and historical writings were not documented, which has led to insufficient research on the myths of the Haya. This article examines the themes constructed through artistic elements in Haya myths. The rationale for this investigation is that artistic elements in literary works have often been studied in a general sense without clarity on how these elements shape themes, especially in the myths of the Haya. Data for this article were collected through interviews. The main discussion is guided by the Reader-Response Theory as developed by Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish (1980), James Tompkins (1980), Hans Robert Jauss (1982), and Robert Holub (1994) in the collection and analysis of the study data. The findings indicate that artistic elements in Haya myths serve as vehicles for constructing key themes. These include the use of traditional tools during meals, the value of possessions, the decline of moral standards, cultural preservation, fertility and reproduction, bride wealth, and compassion toward people in need.
Keywords: Art, Haya, Myths, Themes
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2025 Farida Hassan Kyabalishanga, Joviet M. Bulaya, Leonard Bakize

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.

