Masuala ya Ekolojia katika Bunilizi Teule za Fasihi ya Watoto ya Kiswahili Ikisiri
DOI:
https://doi.org/10.51317/fg87dq15Keywords:
Ekolojia, fasihi ya watoto, mabadiliko ya tabianchi, uhakiki wa kiekolojiaAbstract
Makala hii inalenga kuchunguza mchango wa fasihi ya watoto ya Kiswahili katika kukuza uelewa wa kiekolojia kwa kuchanganua bunilizi teule za Fisi Mtunza Miti (Kobia, 2008), Sifuri Nyani Mtalii (Matundura, 2017) na Kijiji cha Ukame (Babusa, 2020). Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia ya Glotfelty na Fromm (1996). Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makinifu na kuchambuliwa kwa kutumia uchambuzi wa matini. Utafiti ulitumia muundo wa kimaelezo na mbinu ya utafiti wa kimaktaba, huku data zikiwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo yalibainisha kuwa bunilizi teule zimeangazia vyanzo vya mabadiliko ya tabianchi, athari zake na mikakati ya kukabiliana nazo. Vyanzo vilivyojitokeza ni pamoja na uzalishaji wa makaa na ukataji wa miti, huku athari zikihusisha ukame, ongezeko la joto duniani, uhaba wa chakula na vifo vya viumbe hai. Aidha, bunilizi hizo zimesisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira kama wajibu serikali na wa kila mwanajamii. Makala hii inahitimisha kuwa fasihi ya watoto ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ya kujenga mwamko na uwajibikaji wa kimazingira miongoni mwa watoto. Hivyo, inapendekezwa kuwa waandishi wajumuishe maudhui ya kiekolojia katika kazi zao, walimu watumie bunilizi hizo kama nyenzo za kufundishia na wadau wa elimu waimarishe ujumuishaji wa masuala ya mazingira katika mitaala. Utafiti huu una umuhimu katika kuonesha nafasi ya fasihi ya watoto ya Kiswahili katika kuelimisha jamii kuhusu changamoto za kimazingira na kuhamasisha utunzaji endelevu wa mazingira.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Martin Karani Ndeke, Shadrack Kirimi, Mary Kanyua

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.