Nafasi ya Emoji katika Kujenga Maana za Kipragmatiki katika Diskosi za Kidijitali za Kiswahili
DOI:
https://doi.org/10.51317/pt5cpp81Keywords:
Diskosi za kidijitali, emoji, ishara za kidijitali, mitandao ya kijamii, pragmatikiAbstract
Ikisiri
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa emoji katika ujenzi na ufasiri wa maana za kipragmatiki katika diskosi za kidijitali za Kiswahili. Ingawa matumizi ya emoji yameongezeka katika mawasiliano ya mitandao ya kijamii, bado haijaelezwa kwa makini namna emoji zinavyoashiria msimamo wa mwasilishaji, kuimarisha kauli, kupunguza au kuongeza utata na kutekeleza matendo ya usemi kwa kuzingatia muktadha na dhamira ya mtumaji. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umuhimu ya Sperber na Wilson (1995) na kutumia muundo wa kimaelezo. Data kuu zilijumuisha emoji 285 za aina 11 zilizokusanywa kimakusudi kutoka katika diskosi za Kiswahili kwenye WhatsApp na X. Aidha, washiriki 50 waliteuliwa kimakusudi ili kufasiri na kuthibitisha maana za emoji kulingana na muktadha. Data za ziada zilikusanywa kwa kutumia dodoso, mahojiano na majadiliano ya makundi lengwa. Emoji 285 zilitumika katika uchanganuzi mkuu, huku maoni ya washiriki yakisaidia ufasiri wake. Data zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yalionyesha kuwa maana za emoji hujengwa kupitia mwingiliano wa vipengele vya kiisimu, kiutamaduni, kisemiotiki, kiteknolojia na kimwingiliano. Emoji zilibainika kuashiria mtazamo na dhamira ya mwasilishaji, kuimarisha au kurekebisha nguvu ya kauli, kutekeleza matendo ya usemi na kuelekeza ufasiri kulingana na muktadha. Utafiti huu unachangia uelewa wa emoji kama rasilimali za kipragmatiki na kutoa msingi wa tafiti zijazo kuhusu uchakataji wa lugha asilia kwa kutumia akili unde na maendeleo ya lugha za Kiafrika katika teknolojia ya kisasa.
Abstract
This study examined the contribution of emojis to the construction and interpretation of pragmatic meaning in digital Kiswahili discourse. Although emoji use has increased in social media communication, insufficient attention has been given to how emojis signal the communicator’s stance, reinforce utterances, reduce or increase ambiguity, and perform speech acts in relation to context and the sender’s intention. The study was guided by Sperber and Wilson’s (1995) Relevance Theory and adopted a descriptive design. The main data comprised 285 emojis from 11 categories, purposively collected from Kiswahili discourse on WhatsApp and X. In addition, 50 participants were purposively selected to interpret and validate emoji meanings in context. Supplementary data were collected through questionnaires, interviews, and focus group discussions. The 285 emojis formed the primary data for analysis, while participants’ views supported their interpretation. Data were analysed and presented descriptively. The findings showed that emoji meanings are constructed through the interaction of linguistic, cultural, semiotic, technological, and interactional factors. Emojis were found to signal the communicator’s stance and intention, reinforce or modify the force of utterances, perform speech acts, and guide interpretation according to context. This study contributes to understanding emojis as pragmatic resources and provides a foundation for future research on natural language processing using artificial intelligence and the advancement of African languages in modern technology.
Downloads
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Nicholas Owino Agull, Mark Odawo Anjejo, Raphael Mwaura Gacheiya

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.