Uainishaji wa Vishazi Tegemezi Katika Sentensi za Kibukusu

Authors

DOI:

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.771

Keywords:

Kibukusu, sintaksia, uainishaji, vishazi tegemezi, X-Baa

Abstract

Makala hii ilichanganua aina za vishazi tegemezi katika sentensi za Kibukusu, lahaja kubwa ya jamii za Kiluhya inayozungumzwa Magharibi mwa Kenya. Licha ya tafiti nyingi kuhusu fonolojia na mofolojia ya Kibukusu, sintaksia yake, hasa vishazi tegemezi, haijapewa umakini wa kutosha. Utafiti huu ulitumia Nadharia ya X-Baa kubainisha aina za vishazi tegemezi vinavyotumika katika mawasiliano ya wazawa wa Kibukusu. Data zilikusanywa kutoka kwa watafitiwa 15, wakiwemo wanafunzi 7, walimu 5 wa Kiswahili na wazee 3, katika Gatuzi Dogo la Sirisia, Kaunti ya Bungoma. Usampulishaji wa kimakusudi na mpokezano ulitumika, huku data zikikusanywa kupitia uchunzaji mahuluti, mahojiano ya kina na midahalo ya vikundi lengwa. Data zilizorekodiwa zilinakiliwa na kuchanganuliwa kimaelezo, na kuzalisha tungo 129. Matokeo yalibainisha aina sita za vishazi tegemezi: kirejeshi, cha mahali, cha wakati, cha sababu, cha masharti, na kishazi cha utangulizi kinachotumia kiambishi nekhanja/nekharakikha. Kishazi hiki cha utangulizi hakijabainishwa katika tafiti za awali za Kibukusu wala katika typolojia pana ya vishazi tegemezi vya Kibantu. Matokeo yanaunga mkono nafasi ya kishazi kirejeshi kama aina muhimu katika lugha za Kibantu, huku yakipanua mfumo wa kawaida wa aina tatu kwa kuonyesha mgawanyiko wa vishazi vielezi katika aina nne na kubainisha aina mpya ya kishazi cha utangulizi. Utafiti unachangia data mpya katika sintaksia ya lugha za Kiafrika na kutoa msingi wa kuhifadhi Kibukusu.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-09-12

Issue

Section

Articles

How to Cite

Uainishaji wa Vishazi Tegemezi Katika Sentensi za Kibukusu. (2026). Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 122-136. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v7i1.771