Uchanganuzi wa matumizi ya lugha ya urejelezi kati ya jamii ya Abagusii na Kipsigis na matokeo yake katika mahusiano yao

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v6i1.455

Authors

Keywords:

dhima, mawazo ganda, rabsha, urejelezi, vurugu

Abstract

SWAHILI

Uchanganuzi huu unahusu lugha ya urejelezi kati ya Abagusii na Kipsigis na mahusiano yao. Matumizi haya ya lugha ya urejelezi hayajafanyiwa tafiti. Utafiti huu una madhumuni yafuatayo: Kubainisha na kueleza lugha ya urejelezi inayotumiwa na jamii ya Abagusii na Kipsigis, athari za lugha ya urejelezi inayotumiwa na jamii Abagusii na Kipsigis na athari zake katika mahusiano yao na mbinu za suluhisho zinazotumiwa na jamii ya hizi kuunda uhusiano bora kati yao. Nadharia ya utafiti ni; Utambulisho wa Lugha za Kikabila inayohusu makabila/mbali za binadamu na mahusiano kati ya jamii, yaani (‘Ethnolinguistics identity Theory’ ELIT). Uchanganuzi huu ulifanyika katika maeneo ya Borabu na Sotik ambapo ni mpaka wa jamii hizi mbili. Sampuli lengwa ni ya kimakusudi na ilihusu wazee wanaume 10 na kina Mama 10 wenye umri wa miaka 60 na zaidi kutoka jamii ya Abagusii na Kipsigis na jumla ya vijana 20 wenye miaka 24 hadi 35 kutoka pande zote za Abagusii na Kipsigis wanaoishi eneo la Borabu na Sotik. Kwa jumla watafitiwa 60 walihusishwa katika uchanganuzi. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo ambapo mtafiti alishiriki na kufanyia unukuzi wa yaliyojiri. Uchanganuzi huu utafaidi katika kuleta suluhu, amani na utengamano miongoni mwa jamii mbali mbali Kenya na kote ulimwenguni na pia umetoa kumbukumbu za marejeleo ambazo wasomi watatumia ili kufanya tafiti nyingine miongoni mwa jamii mbalimbali kwani matumizi ya urejelezi uzua mitafaruku, rabsha na vita miongoni mwa jamii na umetoa kumbukumbu ambazo serikali kuu na kaunti zaweza kutumia ilikuleta suluhu miongoni mwa jamii wakati wa mitafaruku.

ENGLISH

This study investigated referencial language, that is used by the Abagusii to refer to the Kipsigis and the referencial language used by the Kipsigis to refer to Abagusii. The study investigated the implication of referencial language on the relationship of the two enthnic groups.The study was guided by the following objectives: To identify and explain the referencial language used by Abagusii and Kipsigis to refer one another, to explore the implication of referencial language used and to evaluate how an agreeable relationship between Abagusii and Kipsigis is created as a result of use of referencial language. The study was guided by Ethnolinguistic identity theory (ELIT). This was a qualitative study, a case study perspective. It was carried out in Sotik- Borabu. The target population for the study was 10 old men and 10 old women aged 60 years and above from both communities and 20 youths aged 24 years to 35years from both communities living around the border, in total a sample size of 60 people. Data was analysed and presented by description. It was discovered that the use of referential language cause conflict and war between neighboring communities and therefore there is need to develop a policy to curb this vice. This study will generate knowledge that will contribute to Education sector, Discourse Analysis and to county commisioners who are administrators in the County, National Council for Conflict Resolution Commission, Research in Discourse and Conflict Management.

Key words: Reference, bad thoughts, role, commotion, riot.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2024-01-23

How to Cite

Nyaigoti, K. P., Kitetu, C., & Taib, A. H. (2024). Uchanganuzi wa matumizi ya lugha ya urejelezi kati ya jamii ya Abagusii na Kipsigis na matokeo yake katika mahusiano yao. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 5(1), 1–10. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v6i1.455

Issue

Section

Articles