Kutathmini mitindo mbalimbali ya kisanaa ilitumiwa katika michezo ya mashindano ya shule za upili yanayohusu ugonjwa wa ukimwi

Authors

  • Michael Kiguta Chuo Kikuu Cha Egerton, Kenya.

DOI:

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v4i1.363

Keywords:

mageuzi, sentensi sahili

Abstract

Utafiti huu ulilenga kutathmini mitindo mbalimbali ya kisanaa ilitumiwa katika michezo ya mashindano ya shule za upili yanayohusu ugonjwa wa ukimwi. Nadharia ya semiotiki ilitumika katika utafiti huu. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyokuwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia vigezo mbalimbali vya matumizi ya lugha, maudhui na mbinu Michezo ya shule za upili ni mifupi mno (dakika 35 pekee), kwa hivyo kulihitajika mbinu za kimtindo na kimuundo ambazo zingeweza kusaidia kuwajenga wahusika na msuko wa hadithi uweze kuaminika. Tamthilia ya Majuto ilitumia maonyesho mengi mafupi mafupi ambayo hayakusaidia kuwajenga wahusika kikamilifu. Ingelifaa kama mtunzi angetumia onyesho moja na kuturudisha nyuma ya matukio kupitia mbinu rejeshi.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2022-04-25

How to Cite

Kiguta, M. (2022). Kutathmini mitindo mbalimbali ya kisanaa ilitumiwa katika michezo ya mashindano ya shule za upili yanayohusu ugonjwa wa ukimwi. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 4(1), 434–439. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v4i1.363

Issue

Section

Articles