Maudhui Yaliyotumiwa katika Utunzi wa Michezo ya Kuigiza kuhusu Ukimwi Katika Mashindano ya Sanaa za Shule za Upili.

  • Michael Kiguta Laikipia University, Kenya.
Keywords: michezo ya kuigiza, ukimwi, Sanaa, shule za upili.

Abstract

Utafiti huu ulilenga kutambua maudhui yaliyotumiwa katika utunzi wa michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyokuwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia vigezo mbalimbali vya matumizi ya maudhui. Makala hii ilibaini kuwa watunzi walitumia maudhui mbalimbali kukuza mada ya ukimwi. Baadhi ya maudhui ambayo yalitumiwa yalikuwa ya: mila na utamaduni, uhafidhina, asasi za ndoa, utabaka, utamauushi, uana, malezi, ufuska, uzinzi na kadhalika. Maudhui ulitumiwa kubeba ujumbe kuhusu ukimwi. Utafiti huu ulipendekeza kuwa maudhui yaliyojadiliwa yangefaa kuwa katika tajriba ya vijana ya  kila siku, maudhui ya ukimwi yangelijadiliwa bila kutumia mbinu ya kitanzia, ingekuwa bora kama tamthilia zingelijadili jinsi ya kuishi na waathiriwa wa ukimwi badala ya kuwatenga kama ilivyokuwa katika tamthilia ya Majuto, tamthilia ingetumika kwa njia ya ushawishi kuhusu ugonjwa wa ukimwi badala ya kulaumu na kukemea, mtunzi angeonyesha kuwa maafa si suluhu la matatizo bali ni kutorokea hali ngumu kwa njia ya kifantasia, ingekuwa bora kwa mtunzi kumuondoa katika tamthilia nzima kwa kuwa alifanaya kazi ya mtunzi iwe na udhaifu kisha kulihitajika watunzi wengi wa shule za upili wajitokeze ili tamthilia itumike vilivyo kama chombo mahsusi cha upashanaji wa ujumbe dhidi ya ukimwi.

Published
2022-04-20
Section
Articles