Kuchanganua Aina za Mageuzi katika Maneno ya Sentensi Sahili ya Ekegusii.

  • Wilfrida Kemuma Mount Kenya university, Kenya.
Keywords: Sintaksia Finyizi, kiima, kiarifu, kirai.

Abstract

Utafiti huu unachanganua aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo. Data ilikusanywa maktabani kutumia kifaa cha kudondoa data, kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii. Ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi, mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa. Mbinu za maelezo zilitumika katika uwasilishaji wa data. Mchakato hufanywa kwa kufuata kanuni mahsusi zinazoitwa kanuni geuzi. Ugeuzi unafuata utaratibu maalum, haufanywi kiholela. Katika ugeuzi wa maumbo kuna sharti la ukaribu ambapo hakuna kiambajengo kinaweza kuhamishwa zaidi ya fundo funge mbili kutokana na matokeo ya utafiti huu. Kanuni zingine za uhamisho ni kanuni ya ufungami ambapo muundo wa kijenzi kilichofundwa unahitaji uamuliwe na neno tawala linalofaa. Kuna vilele kanuni ya ulafi, kanuni teta na kanuni hamishe. Mwisho kuna kanuni muundo virai, kanuni geuzi na kanuni za mofofonemiki. Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu aina zingine za mageuzi kama vile, geuzi hamishi swalifu, geuzi hamishi la yambwa tendewa katika lugha hii na hata lugha nyinginezo ili kukuza uwanja wa kisintaksia. Kuna uhamisho unaotokea kwa lugha zingine na siyo katika Ekegusii. Hizi pia zinaweza kufanyiwa utafiti. Tafiti zaidi zinaweza kufanyiwa mada hii kwa kutumia nadharia zingine ili kueleza ikiwa kutakuwa na matokeo tofauti.

Published
2022-04-20
Section
Articles