Matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya Said A. Mohamed
Keywords:
jazanda, fumbo, taswira, kitendawiliAbstract
SWAHILI
Makala haya yanalenga kuangazia matumizi ya jazanda pamoja na uamilifu wake katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya Said A. Mohamed. Jazanda ni matumizi ya maneno ambayo yana fumbo huku yakitoa taswira ya aina Fulani. Said A. Mohamed ametumia jazanda kwa kazi zake kama Amezidi na Kitumbua Kimeingia Mchanga. Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga imetumia mbinu hii kwa njia ya kipekee. Nadharia iliyotumiwa katika kazi hii ni ya Umuundo ambao unasema kuwa kazi ya fasihi inakuwa na muundo ambao unahusisha fani ambazo zitaweza kutumika katika kuwasilisha ujumbe na hivyo maudhui huwa na uhusiano mkubwa sana na fani zitakazotumiwa kuyawasilisha. Utafiti ulifanywa maktabani kwa kuchambua Kitumbua Kimeingia Mchanga, vitabu tofauti na makala mitandaoni. Nakala hii ilipata matokeo kuwa kichwa cha kitabu hiki ni jazanda, pia, kulikuwa na jazanda ya bahari na yale yaliyokuwa yakifanyika kwenye bahari. Jazanda zote zilizotumika ziliweza kuendeleza maudhui kama vile: Mapenzi miongoni mwa vijana, Ndoa, Elimu, Mahusiano katika familia na jamii, Utamaduni na Dini. Uamilifu wa jazanda ni kudhihirisha jinsi mabadiliko yameathiri vijana na hivyo kwenda kinyume na utamaduni na wazee.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2022 Matthew Kwambai

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.

