Sifa Za Kiuhalisiaajabu Katika Riwaya Nne Teule Za Watoto

  • Ruth Wangari Mwai; Dr. Ntiba Onesmus Gitonga
Keywords: Uhalisiajabu, fasihi ya watoto, fantansia.

Abstract

Utafiti huu unakusudia kutathmini sifa za kiuhalisiaajabu katika riwaya nne teule za watoto ambazo ni: Mama wa Kambo (2005) ya Catherine Kisovi, Karamu Mbinguni (2002) ya Njiru Kimunyi, Mkasa wa Fumo Liyongo (2001) ya Bitugi Matundura na Chura Mcheza Ngoma (2001) ya Rebecca. Mtafiti aliteua riwaya nne za watoto kwa kutumia sampuli makusudi. Riwaya hizi ni sehemu ya riwaya hamsini (50) zilizokusanywa zenye data mwafaka na ni baadhi ya miongoni mwa zile ambazo zilipendekezwa na kupitishwa na ile iliyokuwa Taasisi ya Elimu nchini Kenya (K.I.E.) kusomwa na wanafunzi katika darasa la nne hadi la nane na ziliweza kupatikana kwa urahisi kwa madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani. Mtafiti alitumia mbinu ya utafiti ya uchanganuzi wa yaliyomo kama utaratibu wa utafiti wa maandishi. Mtafiti alikusanya data ya kimsingi maktabani. Baadhi ya mihimili yake ndiyo ilitumiwa katika uchanganuzi wa data iliyokusanywa. Pia mtafiti alitathmini vitabu husika na kudondoa data iliyohitajika. Jumla ya riwaya nne zilizoandikwa kwa ajili ya watoto zilitumiwa kupata data iliyotakikana katika uchanganuzi. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Hatimaye, data iliyokusanywa ilichanganuliwa. Utafiti huu ulibaini kuwa Kuna matukio ya kiajabu yaliyotumiwa katika riwaya hizi nne za watoto. Aidha sifa za kihalisiaajabu zimebainika wazi katika riwaya hizi. Kwa mujibu wa makala haya ni bayana kwamba uhalisiaajabu umetumika katika riwaya hizi kwa madhumuni ya kuendeleza masuala ibuka kwa hadhira ya watoto.

Published
2020-10-31
Section
Articles