Kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v4i1.357

Authors

  • Wilfrida Kemuma Mount Kenya University, Kenya

Keywords:

muundo wa maneno, sentensi sahili

Abstract

Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data ulitumika katika kusanya data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumika kwa lengo la kupata sentensi ambazo hudhihirisha mageuzi. Data iliwasilishwa kwa njia za maelezo. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa muundo wa sentensi unahusu mpangilio wa viambajengo katika sentensi. Muundo wa virai ya sentensi sahili ya Ekegusii unategemea majopo ya maneno kisarufi. Majopo ya maneno yaliyotumika katika utafiti huu yanaweza kuainishwa katika makundi wawili: Jopo la leksia na jopo amilifu. Kuna categoria tano za maneno zilizoainishwa katika jopo leksia nazo ni nomino, kitenzi, kielezi, kivumishi na kihusishi. Jopo amilifu hutawaliwa na virai vibainishi, virai vipatanishi na virai shamirisho. Utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti zaidi zinaweza kufanywa kuhusu sentensi ambatano au changamano. Isitoshe, utafiti wa mageuzi unaweza kufanywa kwa lugha nyingine ili kueleza iwapo kuna matokeo tofauti.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2022-04-15

How to Cite

Kemuma, W. (2022). Kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 4(1), 374–398. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v4i1.357

Issue

Section

Articles