Kutathmini Vipengele vya Lugha Vilivyotumiwa katika Michezo ya Kuigiza Kuhusu Ukimwi katika Mashindano ya Sanaa za Shule za Upili.

  • Michael Kiguta Laikipia University, Kenya.
Keywords: Vipengele vya lugha, michezo ya kuigiza, ukimwi, sanaa za shule za upili.

Abstract

Utafiti huu unalenga kutathmini vipengele vya lugha vinavyotumiwa katika michezo ya kuigiza kuhusu ukimwi katika mashindano ya sanaa za shule za upili. Nadharia iliyotumiwa ilikuwa ya umaumbo. Maeneo ya utafiti yalitokana na uchunguzi wa michezo miwili, ambayo ilikuwa: Chozi (2001) na Majuto (2001). Tulitumia michezo kama sampuli iliyowakilisha michezo yote ya Kiswahili iliyo’uwa na mada kuhusu ukimwi. Uteuzi ulitokana na sababu kuwa ulihusu vipengele vya kimsingi kama vile: uhusika, mandhari, jukwaa, kitendo, ploti, lugha maleba na jumuiya. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktabani ulitumia hadhira tuli ya kimaandishi. Data zilizokusanywa kutoka nakala za michezo ziliainishwa kupitia kigezo cha matumizi ya lugha. Ulitafiti huu ulibaini kuwa lugha ya kisanii ilitumiwa katika tamthilia za shule za upili. Lugha iligawanywa kwa mifumo ya mbinu za kiishara na viambajengo vya umuundo. Mifumo ya ishara, maana ya lugha ya kiisimu na taashira za lugha zilitumiwa kujenga tamthilia. Tafiti hii inapendekeza tamthilia kujengwa vizuri kwa njia ya kisanaa kwa kutumia lugha yenye mvuto na mnato kusababisha ujumbe uliofaa, vile vile, wasanii wanahitaji kufanya utafiti mkubwa zaidi kuhusu sanaa ya lugha kwa kuwa ndiyo sehemu ya umuundo na unahitaji ufundi mkubwa.

Published
2022-03-31
Section
Articles