Sababu za Kudondoshwa kwa Fonimu za Likwidi katika Maneno Teule.

  • Evans Kiplimo Cheruiyot Kenyatta University, Kenya.
Keywords: Urahisishaji, utashi wa wazungumzaji, tija, sheria ya uziada na uzuiaji wa sheria.

Abstract

Utafiti huu umelenga kuchunguza sababu za kudondoshwa kwa fonimu za likwidi katika maneno teule. Uchanganuzi huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi. Utafiti huu umetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kupitia kwa mbinu za kusoma na kudondoa. Ili kushughulikia tatizo la utafiti kikamilifu, utafiti huu ulitegemea aina tatu ya data. Kwanza, data ya maumbo yaliyopangwa upya kwa matumizi ya mbinu linganishi na uundaji ndani. Pili, data kutoka kwa Kamusi Kuu ya Kiswahili. Data hii iliteuliwa kimaksudi kwa sababu inaweza kutosheleza katika kushughulikia tatizo la utafiti. Data ya makala hii imechanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Makala hii ilibainisha kuwa ni vigumu kutenganisha vichocheo na sababu kamili za mabadiliko ya lugha. Pili, athari za mabadiliko ya lugha zinaweza kuingizwa kama maelezo ya sababu za mabadiliko ya lugha. Tatu, ilikuwa vigumu kubainisha mipaka baina ya sababu za kiisimu na kiisimu-jamii. Utafiti huu ulihitimisha kuwa kuwa mabadiliko mengine kama vile uchopekaji hutokea katika kiwango cha mofolojia ili kurekebisha makosa ya kimuundo katika lugha yanayosababishwa na badiliko la kwanza. Kando na haya, makala hii ilionyesha kuwa sheria ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi haina tija katika Kiswahili cha sasa. Utafiti huu unapendekeza kuwa Kuzuia uhomonimia na kuwepo kwa masalio ya kiisimu ni baadhi ya sababu zilizotolewa kueleza uzuiaji wa sheria.

Published
2022-01-31
Section
Articles