Mabadiliko Katika Uteuzi wa Majina ya Koo Miongoni mwa Wazinza Nchini Tanzania.

  • Tibezuka B. Clementina; Lina Akaka; Jane Maithya. (1.2.3) Laikipia University, Kenya.
Keywords: Majina ya Koo, Mila na desturi, Utamaduni wa jamii.

Abstract

Makala hii inachambua mabadiliko yaliyopo katika uteuzi wa majina ya koo miongoni mwa Wazinza na sababu zinazopelekea mabadiliko hayo katika utoaji wa majina kwa jamii ya Wazinza. Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile. Mila na desturi za jamii ni mambo ya kimsingi ya kuzingatia wakati wa kuteua majina, hata hivyo mila hizi zimepuuzwa kwa miaka ya hivi karibuni katika jamii ya Wazinza hivyo kupelekea kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika uteuzi wa majina ya koo kwa kutofuata mila na desturi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Makutano na Mwachano iliyoasisiwa na Giles (1982). Mtafiti alitumia mihimili mitatu ya nadharia ya Makutano na Mwachano. Sampuli za utafiti ziliteuliwa kwa kutumia mbinu za kimaksudi na kuelekezwa. Watafitiwa kumi na nane wenye umri wa kati ya miaka 25-90 walichaguliwa. Ukusanyaji wa data uliongozwa na miongozo miwili ya maswali; mmoja wa mijadala ya vikundi lengwa na mwingine wa mahojiano ya kina. Baadhi ya mabadiliko haya ni kama vile; athari za utandawazi, elimu, dini, ndoa, tamaduni za kigeni, lugha za kigeni na watu mashuhuri katika jamii.

Published
2021-10-30
Section
Articles