Mitindo na Lugha ya Uwasilishaji katika Nyimbo za Jando za Jamii ya Watachoni Kutoka Kenya

  • Makhakha, Richard Iyaya; Prof. Nabea Wendo; Dkt. Gwachi J. Mayaka
Keywords: uwasilishaji, nyimbo za jando, Nadharia, umuundo.

Abstract

Utafiti huu ulilenga kutathmini mitindo ya uwasilishaji na lugha inayojitokeza katika nyimbo za jando katika jamii ya watachoni wa kaunti ya bungoma. Nadharia ya baada ya umuundo ya Derrida (1966) ilitumika katika utafiti huu, nadharia hii ilitumika kwa mkamilishano na ya ubabe-dume ya Maclennes (1998).  Utafiti huu ulilenga watahiriwa, wazazi, wanaume Watachoni, wanawake Watachoni na viongozi wa shughuli za jando ya Watachoni wanaotumia nyimbo za jando.  Sampuli kusudio pamoja na nasibu tabakishi zilitumika. Jumla ya nyimbo 16 za nyimbo (nyiso na maghani) za jando zilitumika na watafitiwa 45 walirejelewa. Deta iliyokusanywa ilirekodiwa kwenye kanda na video, ikaandikwa, ikachanganuliwa na kutafsiriwa kutoka lugha ya Kitachoni hadi lugha ya utafiti-Kiswahili kisha kuwasilishwa. Utafiti huu ulitumia mbinu za uchunzaji nyanjani, mahojiano, mashauriano na wasimamizi pamoja na uainishaji wa habari kutokana na vyombo vya habari. Vifaa kama vile kamera za picha tuli na za kunasa sauti na video na data kuziwasilisha kwa njia ya maelezo, majedwali na picha tuli. Utafiti huu uligundua kuwa mitindo na lugha inayotumika katika uwasilishaji wa nyimbo za jando ndiyo inayoyafanya kukidhi mahitaji ya tohara hii pamoja na kuipa upekee wake. Utafiti huu ulihitimisha kuwa Viongozi wa shughuli za jando wanafaa wapitishiwe katika semina za mara kwa mara kuangazia na kuimarisha utendaji wao katika uteuzi wa matini, mitindo na lugha mwafaka za utoaji mafunzo kupitia nyimbo za jando katika jamii ya Watachoni. Utafiti huu unapendekeza kuandaliwe warsha kwa mahafala wa jando kila baada ya miaka minne ili kuwahamasisha kuhusu kanuni, mitindo na dhima za nyimbo katika shughuli za jando ya jamii ya Watachoni.

Published
2021-05-31
Section
Articles