Nafasi ya fasihi simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria: Mfano wa uendeshaji kesi za kitamaduni miongoni mwa Babukusu

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.176

Authors

  • Winnie Musailo Wekesa Chuo Kikuu cha Masinde Muliro, Kenya
  • Fred Wanjala Simiyu Chuo Kikuu cha Kibabii, Kenya
  • Nilson Isaac Opande Chuo Kikuu cha Kisii, Kenya

Keywords:

fasihi simulizi, kisheria, nafasi, ujumbe

Abstract

SWAHILI

Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2020-12-15

How to Cite

Wekesa, W. M., Simiyu, F. W., & Opande, N. I. (2020). Nafasi ya fasihi simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria: Mfano wa uendeshaji kesi za kitamaduni miongoni mwa Babukusu. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 2(1), 173–187. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.176

Issue

Section

Articles